Rais Simba, Evans Aveva kwa
mara ya kwanza amefungua mdomo wake na kulizungumzia suala la sare mbili katika
mechi zao za Ligi Kuu Bara.
Aveva amewataka mashabiki
na wanachama wa Simba kuungana na kuwa pamoja katika kipindi ambacho alikiita
hawajapoteza wala kufanya vizuri.
Lakini akaenda mbali zaidi
na kusema anamuamini Kocha Patrick Phiri, hivyo wampe muda kidogo kwa kuwa
wanapita kwenye kipindi cha mpito.
“Hatujafanya vibaya wala
kufanya vizuri, sare mbili na hakuna mchezo tuliopoteza.
“Ni suala la kujipanga ili
kuangalia tutafanya nini katika mechi zinazofuatia.
“Uongozi una changamoto
nyingi, utaona tulifanya kila linalowezekana kwenye uchaguzi.
“Baadaye kwenye usajili,
lakini sasa bado mambo hayajakaa vizuri, ni suala la kupambana tu,” alisema
Aveva.
Simba imeanzia nyumbani
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar lakini mechi zake zote mbili imetoka sare.
Ilianza sare ya 2-2 dhidi
ya Coastal na mechi ya pili ikatoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Moro. Mechi zote
mbili wageni wakisawazisha katika kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment