Pamoja na kupoteza mechi
yao ya pili kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, Ndanda FC wametamba
bado wana uwezo wa kufaya vema.
Kocha wa Ndanda FC, Denis
Kitambi amesema kikosi chao kina nafasi ya kuendelea kutamba.
“Tulianza vizuri kwa
ushindi mkubwa zaidi wa mabao manne dhidi ya Stand.
“Lakini tukapoteza dhidi ya
Mtibwa Sugar, hii inaonyesha ligi ni ngumu kiasi gani.
“Haina maana kwamba
tutashindwa kufanya vema, tunajirekebisha kama wenzetu na baada ya hapo
tunaendelea kupambana.
“Tunajiamini kwa maana ya
uwezo na kwenye makosa tunajipanga upya,” alisema Kitambi.
Ilianza mechi yake ya
kwanza ya ligi kwa kishindo kwa kuitwanga Stand United kwa mabao 4-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment