JAJA |
Nahodha
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro, ameibuka na kusema kuwa mshambuliaji wao
Mbrazili, Geilson Santana ‘Jaja’, ana uwezo mkubwa zaidi ya Mrundi wa Simba,
Amissi Tambwe.
Jaja
yupo kwenye wakati mgumu kutokana na kutoaminiwa na mashabiki wa klabu hiyo
wakidai kuwa ni mzito na hawezi kupiga chenga.
Akizungumza
jijini Dar, Cannavaro amesema, Jaja hapaswi kubezwa licha ya kuwa hajui kupiga
chenga na anahitaji muda kwani ni zaidi ya mshambuliaji wa Simba, Amissi
Tambwe.
Alisema
Jaja atakuwa mchezaji mzuri akishazoeana na wenzake na kwamba akiwa mbele ya
lango ni ngumu kukosa bao.
“Huyu
ni zaidi ya Tambwe sema watu wanataka vitu haraka, mpeni muda mtamuona tu,”
alisema Cannavaro.
Hata
hivyo Cannavaro hakufafanua zaidi ubora aliouona wa Jaja hadi kumzidi Tambwe
raia wa Burundi ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora akiwa na mabao 19.
Jaja
tokea atue Yanga, ameishacheza mechi nne za kirafiki na kufanikiwa kufunga
mabao mawili, kila moja likiwa la ushindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment