Kikosi cha JKT Ruvu ya mkoani Pwani, kinaamini kiko sawa kwa ajili ya mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara na kinatata kubeba pointi tatu za kwanza.
Mechi yao ya kwanza ya ufunguzi itakuwa ugenini dhidi ya Mbeya City wanaodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Ltd kupitia betri zake za RB.
Maafande
hao tayari wamecheza michezo
kadhaa walipokuwa katika mashindano ya majeshi yaliyokuwa yakifanyika visiwani
Zanzibar.
Kocha
msaidizi wa maafande hao, Azishi Kondo, amesema maandalizi bado yanaendelea kwa kuwa
timu ipo kambini baada ya kurejea kutoka Zanzibar ilipokuwa ikishiriki
mashindano maalum ya majeshi.
“Maandalizi
bado yanaendelea, baada ya timu kurejea kutoka Zanzibar imeingia kambini
Jumatatu (juzi), kuweka mipango mizuri kuhakikisha tunafanya vyema katika
mchezo wetu wa kwanza ugenini.
“Tunaijua
vizuri Mbeya City ni timu ngumu, hasa inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani
lakini mimi niwatumie salamu tu kwamba soka ni mchezo wa uwanjani siyo maneno,
acha wao wapige kelele mwisho wa siku dakika tisini ndizo zitakazoamua,”
alisema Kondo.
0 COMMENTS:
Post a Comment