Kocha Mkuu wa Brazil, Dunga
hataki mchezo na beki wa kulia Maicon anaweza kuthibitisha hilo.
Dunga amemtimua Maicon
aliyewahi kucheza Man City na Inter Milan kutokana na utovu wa nidhamu.
Alikuwa katika kikosi cha Brazil
kilichoitwanga Colombia bao 1-0 katika mechi ya kirafiki nchini Marekani.
Wakati inajiandaa na mechi
nyingine ya kirafiki Ecuador, Maicon ’34, ambaye ameichezea Brazil mechi 76
ametupwa nje.
Hiyo ni kuonyesha kwamba
Dunga ambaye amerejea baada ya Fillipe Scorali aliyepigwa 7-1 na Ujerumani
katika mechi yake ya mwisho, hataki mchezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment