September 6, 2014

KADUGUDA AKIMWELEZA PHIRI HISIA ZAKE.

Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Kaduguda, leo alikubali kupoteza zaidi ya dakika kumi kumsubiri Kocha Patrick Phiri.

Kaduguda ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Fat, alilazimika kumsubiri Phiri aliyekuwa akihojiwa na waandishi wa habari ili atoe pongezi zake.

Mara baada ya Phiri raia wa Zambia kumaliza kuhojiwa, Kaduguda alimfuata na kumueleza alivyofurahishwa na mpira katika mechi dhidi ya Gor Mahia ambayo Simba ilishinda 3-0.
“Ingawa ni mechi ya kirafiki lakini huu ndiyo mpira wa Simba, leo nimefurahi sana,” Kaduguda alimwambia Phiri ambaye alionyesha furaha kubwa kumuona.
Wakati Kaduguda akiwa katibu Simba, Phiri alikuwa kocha.

Wote walisalimiana kwa furaha kubwa na kuzungumza machache kabla Kaduguda maarufu kama Simba wa Yuda, kuchukua time zake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic