September 19, 2014


Straika wa Azam FC raia wa Burundi, Didier Kavumbagu amesema hatawasahau walinzi wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani kwa kuwa walimchezea kibabe katika mechi yao ya Ngao ya Jamii, kiasi cha kutaka kumvunja.


Akielezea mechi hiyo iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumapili iliyopita, alisema hakufurukuta kwa kuwa wawili hao walimchezea vibaya muda mwingi wa mchezo. Azam FC ililala kwa mabao 3-0.

“Walikuwa wakinichezea kibabe na kunikaba muda wote kama walivyokuwa wakifanya kwa Kipre Tchetche, lakini sawa, yote yamepita.

“Mungu akipenda tutaonana tena katika ligi kuu, na hapo ndipo nami watakapoona kazi yangu,” alisema Kavumbagu.
Raia huyo wa Burundi ametua Azam FC akitokea Yanga ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico ya kwao Burundi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic