September 19, 2014


Kipa wa Gor Mahia ya Kenya, Fredrick Onyango, amesema kumkaba mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera si kazi lahisi.

Lakini akasisitiza, kama timu inataka kupumua, basi ni kutompa nafasi ya kufanya mambo yake.

Kiongera anatajwa kuwa mmoja wa washambuliaji hatari wanaotarajiwa kutamba katika Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kesho Jumamosi.

Kipa huyo Mkenya amesema, Kiongera ni hatari akiachiwa nafasi. “Wanatakiwa kutompa nafasi ya kucheza na kufanya anavyotaka, wakifanya hivyo tu watakuwa wamemmaliza.
Onyango ambaye alifungwa mabao mawili na Kiongera wakati Simba ilipoitwanga Gor Mahia kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki, amesema Kiongera ana mambo mengi.
“Uwezo wake ni mkubwa, ana kasi, nguvu na anapiga mashuti. Unaweza kusema ana kiula kitu, hivyo kuwa naye makini ni jambo zuri.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic