September 20, 2014


Simba iko katika hatua za mwisho kupata kibali cha kufanyia kazi nchini cha kiungo wake Emmanuel Okwi raia wa Uganda.

Iwapo Simba itashindwa kupata kibali hicho leo, maana yake Okwi hatacheza mechi dhidi ya Coastal Union kesho.
Simba inawavaa Wagosi wa Kaya kesho kwenye Uwanja wa Taifa kwenye mechi yake ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara.
Rais wa kwanza wa Simba, Evans Aveva amethibitisha hilo na kueleza linafanyiwa kazi kwa juhudi kubwa.
Okwi amejiunga na Simba akitokea Yanga ambayo ilimpata kutoka SC Villa ya Uganda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic