Mtibwa imetamba kuwa ushindi wake wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC ilikuwa ni pati ya kuwakaribisha vijana hao kwenye Ligi Kuu Bara.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema Ndanda FC ni makinda na haikuwa lahisi washinde kwa dhidi ya Mtibwa Sugar.
"Nilisema Ndanda ni makinda hakuna aliyeniamini, lakini tuliwafanyia pati kuwakaribisha kwenye ligi kuu.
"Hii ni ligi ngumu hivyo wajue kuwa wanatakiwa kujipanga zaidi na si wakishinda dhidi ya timu fulani wanajua wataishinda na nyingine.
"Wamekuja hapa Manungu na vijana wao yaani mashabiki kwa wingi, lakini nilijua wataondoka kwa majonzi," alijigamba Kifaru.
Katika mechi ya kwanza, Mtibwa Sugar iliitwanga Yanga kwa mabao 2-0, Ndanda FC ikaobomoa Stand United kwa mabao 4-1, hivyo zilikuwa ninakutana timu zilizoonja ushindi katika mechi za kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment