Mshambuliaji wa AS Roma ya Italia, Alessandro Florenzi amepiga bao
na haraka akapanda jukwaani na kwenda kumkumbatia bibi mwenye umri wa miaka 82.
Ilikuwa ni mechi kati ya AS roma dhidi ya Cagliari na wakashinda
kwa mabao 2-0, yote yakiwa yamepigwa na mshambuliaji huyo.
Mara baada ya kufunga mshambuliaji huyo alipanda kasi kwenda juu
ya jukwaa na kumkumbatia bibi huyo.
Huo ulikuwa ni ushindi mwingine wa AS Roma baada ya kuwa
imeiadhibu kwa mabao 5-1 timu ya CSKA Moscow katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment