Kocha Mkuu wa Yanga, Marcimo amesema kikosi chake kipo tayari kwa
ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Aidha, Maximo ameeleza furaha yake kurejea kwa wachezaji wawili,
Jerry Tegete na Andrey Coutinho ambao walikuwa majeruhi.
Lakini akaeleza kusikitishwa na majeruhi Oscar Joshua na Hussein
Javu, hata hivyo akasisitiza waliobaki wako fiti na tayari kuiwakilisha Yanga
vema katika mechi hiyo ya kesho.
Maximo ameiambia SALEHJEMBE mara baada ya mazoezi ya Yanga leo
kwamba anaamini Prisons kwa kuwa walishinda mechi ya kwanza dhidi ya Ruvu
Shooting, watakuwa na morali ya kuendeleza ushindi, hivyo itakuwa ngumu.
Yanga itakuwa na kibarua cha kutaka kujihakikishia kushinda baada
ya kuchapwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment