Wakati Yanga iko katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa
Prisons jijini Dar, uhakika kuwa itawakosa beki wake wa kushoto Oscar Joshua na
mshambuliaji Hussein Javu.
Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Juma Sufiani, wote wawili
wanasumbuliwa na nyama za paja.
“Tumewapumzisha lakini matarajio kuwa wataanza mazoezi mepesi
kuanzia Jumatatu,” alisema.
Joshua alikuwa kati ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha
kwanza cha Yanga kilichoivaa Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Katika mechi
hiyo, Yanga ililala kwa mabao 2-0 dhidi ya wakata miwa hao wa Turiani.
0 COMMENTS:
Post a Comment