September 5, 2014


Baada ya kufanikiwa kutua Simba, kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi hicho, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo bure.


Okwi amesema maneno hayo akimaanisha kuwa yupo tayari kucheza bila hata kulipwa mshahara kwa kudai kuwa hilo suala la fedha siyo tatizo kwake.

Okwi ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga na kusaini kuichezea klabu hiyo kwa miezi sita, amesisitiza kuwa anaipenda Simba na atafanya hivyo pia itakapobidi ili kulinda kiwango chake.

“Unajua sasa hivi nimebadilika na siyo Okwi yule waliyekuwa wakimjua, sitakuwa mtukutu kama ambavyo walikuwa wakinisema mwanzoni, nguvu zangu zote naelekeza kuisaidia timu yangu ya Simba,” alisema Okwi.

Mganda huyo ambaye msimu uliopita alizichezea Etoile du Sahel na SC Villa, ameongeza kuwa anaamini yuko mahali sahihi, hivyo atahakikisha anapambana kuweka kiwango chake kuwa bora.


“Nimefurahi kurejea Simba na kuitumikia timu hii, mshahara siyo tatizo,” alisema Okwi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic