KIONGERA AKIGONGANA NA KADO... |
Picha inaonyesha kipa Shabani Kado akimgonga mshambuliaji Paul Kiongera wa Simba wakati wakiwania mpira,
Kiongera raia wa Kenya aliumia na kutolewa nje, Kado akatibiwa na kumalizia dakika moja iliyobaki.
Sasa Kiongera anaikosa mechi ya Oktoba 12 ya watani wao Yanga ambayo inasubiriwa kwa hamu.
ANAANGUKA BAADA YA KUGONGANA NA KADO AMBAYE ANALIA MAUMIVU PIA... |
Vipimo vilivyotolewa leo kwenye hospitali ya
rufaa ya Muhimbili vimeeleza Kiongera ameumia sana goti lake na tayari
imepitishwa apumzike wiki sita.
Hali hiyo imejulikana baada ya daktari wa
Simba kusafiri na Kiongera hadi Dar es Salaam wakitoka kambini Zanzibar na
kufanyiwa vipimo.
Majeruhi wengine ni Haruna Chanongo ambaye
amebakiza siku mbili kabla ya kurudi uwajani na kuanza mazoezi mepesi na Issa
Rashid maarufu kama Baba Ubaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment