Idara ya Uhamiaji Tanzania,
imetoa tamko la kuwazuia washambuliaji wawili wa Simba, Paul Kiongera raia wa
Kenya na Emmanuel Okwi kutoka Uganda.
Uhamiaji imesema wachezaji
hao hawana kibali cha kufanya kazi nchini.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji,
Abbas Irovya amesema hawaruhusiwi kufanya kazi hadi watakapopata kibali.
“Si kucheza mechi tu,
hawaruhusiwi kufanya mazoezi na Simba kwa kuwa bado hawajapata kibali,”
alisema.
Irovya amesisitiza Simba
kuwasilisha maobi kama inataka kuwatumia katika mechi au kushiriki nao mazoezi.
Pia akashangazwa kuona
wanaendelea kucheza huku Shirikisho la Soka Tanzania likiwa kimya.
Wiki iliyopita Idara ya
Uhamiaji ilisisitiza suala la wachezaji wa kigeni kupatiwa vibali kwa klabu zao
kuwasilisha maombi.
Okwi alikuwa na kibali cha
kufanya kazi nchini lakini kilikuwa kimetafutwa na mwajiri wake wa zamani,
Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment