Mshambuliaji mpya wa
Arsenal, Danny Welbeck, ameibuka shujaa wa England baada ya kufunga mabao yote
mawili na kuipa England ushindi wa 2-0 ikiwa ugenini.
Katika mechi hiyo iliyomalizika mjini Basle, Switzerland, wenyeji wamelala kwa mabao hayo mawili ya Wilbeck katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Euro.
Welbeck alianza kufunga bao lake la kwanza katika dakika ya 59 baada ya nahodha Wayne Rooney kushirikiana vizuri na winga hatari, Raheem Stelring.
Wakati wenyeji wakiwa wanajitahidi kusawazisha, Welbeck tena alitupia bao la pili katika dakika ya 90 na kuihakikishia England ushindi.
Welbeck ametua Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 16 akitokea Man United.
0 COMMENTS:
Post a Comment