September 19, 2014

Kocha Arsene Wenger wa Arsenal amezidi kumtetea kiungo wake Mesut Ozil kwamba anaboronga.
Wenger amesema Ozil hajawa vizuri sana lakini hawezi kuwekwa kwenye kundi la wanaoboronga.

Katika dakika zaidi ya 60 alizocheza katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund alishindwa kung’ara huku Arsenal ikilala kwa mabao 2-0.
Wenger amesisitiza, kiungo huyo atakuwa fiti zaidi baada ya mechi chache zijazo.

Lakini ramani za mchango wake uwanjani katika mechi nne alizocheza, zinaonyesha Ozil ameshuka.
Arsenal imetoa zaidi ya pauni milioni 42 kumnasa, lakini Mjerumani huyo mwenye asili ya Uturuki anaonekana hana mchango wa kutosha.
Ramani hizo zinaonekana kuwa Ozil hana mchango mkubwa na anaonekana amecheza maeneo machache sana uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic