October 9, 2014


Maisha si kitu lelemama, unatakiwa kuwa imara na kuamini ukipambana, ukafanya juhudi, utafanikiwa.

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ,25, sasa analipwa pauni 150,000 (Sh milioni 375 kwa wiki).
Lakini alikuwa akilazimika kukusanya fedha kwa kupata pauni 2.30 (Sh 5,750) kutokana na kuosha magari au kucheza sarakasi hasa kujipindua mbele au nyumba, maarufu kama ‘samasoti’.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake wakati akiwa mtoto kwao Chile.
Katika mahojiano na Daily Express la Uingereza, Sanchez ambaye alitua Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 30 akitokea Barcelona, anasema hakuweza hata kununua kiatu.
“Kiatu changu cha kwanza cha soka nilipata baada ya mama yangu kwenda ofisini kwa Meya wa eneo tulilokuwa tukiishi na kumuomba.
“Siku chache baadaye Meya alikuja nyumbani kwetu na kunikabidhi.
“Nilipata fedha kwa kucheza sarakasi, pia nilijiongezea kipato kwa kuosha magari,” anasema.
Hili linaweza kuwa funzo kwa wanamichezo au watoto wanaochipukia, kwamba hawapaswi kukata tamaa na maisha.

Juhudi na malengo, vinaweza kuwa dira kwenda mbele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic