YANGA WAKIJIFUA MJINI KAHAMA, LEO. |
Kikosi cha Ambassador cha
mjini Kahama kitakuwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya kirafiki itakayopigwa
Jumatano.
Yanga iko katika maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa wikiendi hii kwenye Dimba la Kaitaba,mjini Bukoba.
Mechi hiyo itapigwa kwenye
Uwanja wa Kahama.
Msemaji wa Yanga, Baraka
Kizuguto ameiambia SALEHJEMBE kuwa kweli mchezo huo utakuwepo.
“Ni kweli tuna mechi,
itapigwa Jumatano na baada ya hapo ndiyo tutasafiri kwenda Bukoba, hiyo timu
inashiriki daraja la pili,” alisema Kizuguto.
Mechi hiyo itakuwa ya pili
ya Yanga kirafiki kwa kuwa ilianza kucheza na CDA ikiwa mjini Dodoma na kutoka
nayo sare ya bila kufungana halafu ikasafiri hadi Shinyanga na kuifunga Stand
United kwa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment