October 27, 2014


Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amejigamba na kusema Simba anaifananisha na timu ya daraja la kwanza.

Simba inakutana na Mtibwa Sugar katika mechi yake ya sita ya Ligi Kuu Bara wikiendi hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kifaru amesema wakiwa Mbeya kabla ya kucheza na Mbeya City waliishuhudia Simba ikitoka sare ya mabao 1-1 na Prisons.
“Simba ni timu isiyo na mfumo mzuri, iliyojaza wachezaji wengi wageni wasio na msaada wowote.
“Sisi tunawachukulia kama timu ya daraja la kwanza na tutawamaliza Morogoro pale Jamhuri, watu waje waone,” alisema Kifaru.

Tayari Simba ina sare tano wakati Mtibwa Sugar ndiyo timu inayoongoza kwa ushindi na inaonekana ni tishio zaidi kuliko timu nyingine ya Ligi Kuu Bara kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic