Na Idriss Ally, Mwanza
Kocha John Tegete amesema kikosi chake cha
Toto African kinataka kuendelea kufanya vizuri mfululizo.
Tegete ambaye ni baba mzazi wa Jerry Tegete
wa Yanga, amesema anaamini ana kikosi bora ambacho kinaelewa nini maana ya
ushindi.
Katika mechi iliyopita ikiwa ni ya ufunguzi
wa Ligi Daraja la Kwanza, Toto iliitungua Mwadui ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwa
bao 1-0.
“Vijana wana morali iko juu, sasa wanajua
nikisema ushindi ni muhimu wanaelewa. Tunatakiwa kushinda mfululizo.
“Hauwezi kurejea ligi kuu bila ya kufanya
vizuri, kufanya vizuri ni ushindi, hilo halina mjadala,” alisema Tegete ambaye
ni kocha mkongwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment