JANIS AKIWA NA BAADHI YA WATOTO KWENYE KIKOSI CHA MARSH |
Na
Idriss Ally, Mwanza
Kocha
wa zamani wa Taifa Stars, Sylvester Marsh amepata wafadhili kutoka nchini
Ujerumani.
Wafadhiri
hao watakuwa wakinunua vifaa kwa ajili ya timu yake ya watoto na vijana.
Mmoja
wa wafadhiri hao aliyenijambulisha kwa jina la Janis alisema ufadhili wao ni wa
kulitolea.
“Tutakuwa
tunanunua vifaa, si kwa idadi kubwa kwa asilimia mia.
“Lakini
kadiri ya uwezo wetu kwa kuwa ufadhili wetu si wa makampuni ila ni watu
wanaotaka kujitolea kusaidia na kuendeleza,” alisema.
Marsh
amekuwa akiendelea na mazoezi na kikosi chake mjini hapa.
Wazazi
wameanza kuvutiwa na kuanza kuwapeleka watoto wao kwa wingi kwa kuwa
wanamuamini ni mmoja wa makocha bora kabisa nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment