October 29, 2014

BAHANUZI
Mshambuliaji Said Bahanuzi ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha Marcio Maximo, ameifungia Yanga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ua timu ya Ambassador FC.

Katika mechi hiyo ya kirafiki mjini Kahama, Ambassador wanaokipiga daraja la pili ambao ni wenyeji wa Yanga, walikubali kipigo baada ya Bahanuzi kufunga bao katika dakika ya 41.
Maximo alitumia kikosi chenye wachezaji wengi wanaokaa benchi ambao walipata nafasi ya kucheza.
Huo ni mchezo wa mwisho kabla ya Yanga kuanza safari kwenda Bukoba kuivaa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic