October 29, 2014

MAGURI.
Mshambuliaji Elius Maguri amefunga bao pekee  la Simba katika mechi ya kirafiki leo dhidi ya Lipuli ya Iringa ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, wikiendi mjini Morogoro.

Maguri alipiga bao hilo katika dakika ya 54 akikiongoza kikosi kilichojaa wachezaji wengi ambao hubaki kwenye benchi au jukwaani.
Nyota wengi wa Simba walibaki jukwaani kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati wenzao wakihenyeshana na Lipuli wanaoshiriki Ligi daraja la Kwanza.
Baada ya mechi hiyo, Simba sasa itaanza safari kwenda Morogoro kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic