October 3, 2014

Unaweza kusema ni maswali matano ya Kassim Dewji kwa Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri.

Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Dewji aliibuka kwenye mazoezi ya Simba na kufanya mazungumzo na Phiri pamoja na msaidizi wake, Selemani Matola.
Alichotaka kujua,  unaweza kuangalia maswali haya.

1.   Tatizo la kufunga mabao zaidi?
2.   Vipi mabeki wanaruhusu mabao?
3.   Kwa nini timu haichezi vizuri kipindi cha pili?
4.   Kwa nini Simba haijafunga bao katika kipindi cha pili?
5.   Phiri anataka nini kwa ajili ya mabadiliko?

Kwa kuwa Dewji amewahi kufanya kazi na Phiri, tena kwa mafanikio makubwa, hakuna ubishi maswali hayo yalijibika na wakashauriana.
Dewji anaamini Simba ina kikosi kizuri lakini kuna mambo kadhaa ya kurekebisha.

Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza alimuachia kazi yake Phiri lakini akamsisitiza juhudi na mipango ya uhakika ifanyike kuiangusha Stand United, kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dat.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic