October 3, 2014


AVEVA, KIGOMA&DEWJI.


Baadhi ya viongozi wa kundi la Friends of Simba (Fos), wameamua kuingia mzigoni kuhakikisha kuna mabadiliko kwenye kikosi cha Simba.

Pamoja na Kassim Dewji, pia Mohammed Kigoma alikuwepo kwenye mazoezi hayo.
Mwingine ni Rais wa Simba, Evans Aveva ambaye ndiye mwanzilishi wa Fos.
AVEVA AKIFUATILIA MAZOEZI
Dewji na Kigoma, wao ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba.
Jana walitua mazoezi ya Simba ghafla, wakionyesha wana hamu ya kuona kama kuna tatizo hadi kikosi hicho kupata sare mbili mfululizo.
Katika mazoezi ya Simba Bunju nje kidogo ya jiji la Dar, viongozi hao walifika mazoezini na kufanya mazungumzo na viongozi wa timu.
Pamoja na Kocha Mkuu, Patrick Phiri, msaidizi wake, Selemani Matola, pia walizungumza na baadhi ya wachezaji.
Awali inaelezwa Fos, wameanza uchambuzi wa kina kutaka kujua kama kuna tatizo la malipo, au makundi ndani ya kikosi chao.

DEWJI NA AVEVA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic