Makocha 32 kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar watahudhuria kocha ya ukocha ya ngazi pevu (advance) iliyoandaliwa na
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itakayofanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Oktoba 13 mwaka huu.
Kozi hiyo itakayomalizika Oktoba 25
mwaka huu itaendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) Ulrich Marriot kutoka Shelisheli, na makocha wanatakiwa kuripoti hosteli
za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Oktoba 12 mwaka huu jioni.
Makocha hao ni Ahmed Suleiman Simba
(Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin
(Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman
Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki
Abeid (Geita).
Edna Lema (Morogoro), George Melchior
(Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA),
Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA),
Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).
Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed
Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles
Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi
Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia
Mgambwa (Rukwa).
Makocha
watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za ukocha za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF).
0 COMMENTS:
Post a Comment