Na Mwandishi Wetu
Shindano la ‘Nani Mtani Jembe2’ linalowakutanisha wakongwe
wa Soka hapa nchini Simba na Yanga, limeanza kwa kasi msimu huu, baada ya jana
kuwepo kwa shamrashamra za aina yake katika uzinduzi rasmi uliofanyika katika
viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Msimu huu wa ‘Nani Mtani Jembe2’ unaoendeshwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager- wadhamini wakuu wa timu hizo, ulishuhudiwa Simba
akianza vema katika mchezo wa soka baada ya Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji
Said Tully kuwabuziga Yanga bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa mashabiki wa
Simba na Yanga uliokuwa sehemu ya uzinduzi huo.
Katika mchezo huo wa soka ambao ulionekana kuwa na
ushindani mkubwa, Simba waliwafunga Yanga iliyoongozwa na nahodha wao Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji Mohamed Bhinda huku kwa upande wa danadana Bhinda akimshinda
Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’,huku kwa upande wa
kuvuta kamba
mashabiki wa tiu hizo wakitoka sare.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa timu hizo ‘Kaburu’
wa Simba pamoja na Mohammed Bhinda wa Yanga wote walianza kujigamba kuhakikisha
wanaibuka na kitita cha mil 100 ambacho kimeandaliwa na Kilimanjaro Premium
Lager.
Kaburu alisema, Yanga wameonekana wazi kuanza kushindwa,
baada ya kuwatembezea kichapo cha bao 1-0 na pia kutoka sare ya kuvutana kamba
hasa wakizingatia msimu uliopita wa Nani Mtani Jembe waliwazidi katika kila
idara isipokuwa katika kura zilizopigwa na mashabiki ambapo Yanga
walipigiwa zaidi kura na kuibuka na kitita cha shilingi milioni 98 kati ya milioni
100.
“Hapa imeonekana tumetoka sare katika kuvuta kamba, ila
Yanga kama mnavyowajua wanapenda ubishi, wamevuta kamba wengi zaidi ya sisi
lakini tumewaachia tu na msimu huu tutahakikisha tunachukua pesa zote na
kuwaachia kifuta jasho tu,’alisema Kaburu.
Naye Bhinda aliwataka wanachama na mashabiki wa Yanga
kuhakikisha wanaitendea haki Nani Mtani Jembe2 hii ili Yanga iwagalagaze Simba,
kwa kuwa msimu uliopita waliwawaonea huruma Simba na kuwapa nafasi ya kuwafunga
mabao 3-1 baada ya kuona wamezidiwa katika kuvutana.
“Sisi bwana hatuna shida na hawa watani zetu ndio maana
tukawaleta wachezaji kutoka katika kitovu cha soka Brazil na bila ya kuwaleta
sisi Simba wangetoa wapi nafasi ya kuwaona Wabrazil wakisakata kabumbu
Tanzania,”alisema Bhinda.
Alisema kwa kila bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye
ujazo wa milita 500 ambayo mteja atanunua ataona namba maalum na ataandika jina
la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo na atatuma kwenda namba
15415 na kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 10,000 kwenye
akaunti ya klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh.
10,000.
“Msimu huu ni wa kipekee sana maana tumeona bora
atakayefungwa siku ya mechi ya Nani Mtani Jembe walau apate kifuta jasho cha sh
mil 5 huku mshindi akipata milioni 15. Klabu itanufaika, wachezaji watanufaika
na mashabiki watanufaika. Sasa ni kazi kwenu viongozi kuwahamasisha mashabiki
wa timu zenu,”alisema Kavishe.
0 COMMENTS:
Post a Comment