Baada ya kuanza na sare tatu mfululizo katika Ligi Kuu Bara, sasa Simba inatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Afrika Kusini.
Simba inataka kwenda Afrika Kusini kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wake wa jadi Yanga.
Mechi hiyo itapigwa Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
"Kila kitu kipo kwenye hatua ya mwisho, timu inaweza kuondoka nchini kesho kwenda Afrika Kusini.
"Itakaa Johannesburg na kurudi nchini siku chache kabla ya mechi," kilieleza chanzo cha uhakika.
0 COMMENTS:
Post a Comment