Mshambuliaji Mrundi wa Simba, Amissi Tambwe, amefunguka kuwa
amejipanga kuhakikisha anatetea kiatu chake cha dhahabu alichokitwaa msimu
uliopita.
Tambwe msimu uliopita aliibuka Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara baada
ya kufunga mabao 19, lakini msimu huu amecheza mechi mbili na kufunga bao moja.
Tambwe alisema bado hajakata tamaa kwani muda bado kwa hiyo anaamini
atafanya vizuri na kutengua kauli ya watu wanaosema msimu huu atapoteza kiatu
hicho.
“Unajua nashangaa sana watu wanavyosema sitaweza kutetea kiatu
changu kwani ukiangalia ndiyo kwanza tumecheza raundi mbili tu hivyo muda bado,
lakini ninawaambia nitatetea tena msimu huu,” alisema Tambwe.
Tambwe ambaye tayari amefunga bao moja katika mechi mbili, anaamini
anaweza kufanya vizuri tofauti na wengi wanavyodhani.
Kabla ya kuanza kwa msimu mpya, uongozi wa Simba nusura umteme
Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Okwi, lakini wadau wakacharuka.
0 COMMENTS:
Post a Comment