October 3, 2014


Timu ya Global FC, leo Ijumaa inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar.


Global itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya timu ya Wizara ya Sheria na Katiba kwa kufungwa mabao 4-1.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Global FC, Nassor Gallu ‘Bonge la Mtu’ amesema kikosi chao kipo kwenye hali nzuri ambapo kimeongezwa nguvu baada ya beki wao aliyekuwa majeruhi, Sweetbert Lukonge kupona na leo anatarajiwa kushuka dimbani.

“Tunacheza na Royal ambapo tunatarajia mchezo huo utakuwa mzuri na wa kuvutia ambapo tutataka kuibuka na ushindi ili kulipiza kisasi baada ya kupoteza mchezo uliopita tulipocheza na Wanasheria,” alisema Gallu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic