UGANDA wamepoteza nyumbani katika mechi yao
ya makundi kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika (Can) kwa kufungwa na Togo
kwa bao 1-0.
Kwa rekodi zao inaonyesha kwenye mashindano
makubwa walipoteza nyumbani mara ya mwisho mwaka 2004, miaka kumi iliyopita.
Maana yake sasa wanajipanga kurekebisha mambo watimize ndoto ya kucheza Kombe
la Mataifa Afrika.
DR Congo wamefungwa na Sudan wameitwanga
Nigeria bao 1-0, DR Congo pia wamepoteza kwa bao 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya
Ivory Coast kama ilivyo kwa Malawi ambao wamefunga 2-0 na Algeria pia wakiwa
kwao.
Waliopoteza wote watakuwa wanajipanga,
walioshinda pia watajiandaa zaidi ila usisahau jambo kwamba nchi zote
nilizozitaja ni jirani zetu au kutoka kwenye uanda wetu, viko busy kuwania
kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Wakati nchi hizo zinapambana kupata
mafanikio sahihi katika mchezo wa soka, Shirikisho la Tanzania (TFF), liko busy
kupambana kuwaziba mdomo wote wale ambao wanaonekana kipingamizi kulizuia
kwenda kwenye njia ambayo si sahihi.
TFF kupitia sekretarieti yake ambayo
imechukua majukumu ya kamati ya utendaji sasa inafanya kila linalowezekana
kufungia wadau wote wenye uwezo wa kupambana na kupinga mapungufu yao pia
kuwaogopesha wengine waliotaka kuwaunga mkono.
TFF sasa iko kwenye mikakati ya kubadili
kanuni ili iweze kuibana bodi ya ligi isiwe na meno, iwe ni ile ambayo
itaendesha mambo yake kwa uoga.
Inawezekana kabisa kuvibana hata vyombo vya
habari ambavyo vinaonekana kushangazwa au kushitushwa na uongozi huo ambao
ndiyo mpya lakini umefeli, umeonyesha hauwezi na sasa unapambana nje ya njia
sahihi ya kuleta maendeleo.
Kikubwa ni kwamba TFF inaendesha mpira wa
Watanzania na hata ifanye lipi haiwezi kukwepa kukosolewa kwa kuwa hakuna
anayeimiliki TFF ambayo ni taasisi ya umma.
Kulazimisha mambo sasa ni kujidanganya tu
kwa kuwa ukweli wa kila kitu uko wazi lakini nina ushauri na sitachoka kushauri
hata kama kutakuwa na juhudi za kujaribu kunizima, nitasema tu, hata kama
nimelala.
Kwamba TFF, lazima ianze kutafakari kwamba
Watanzania wamechoka kufeli, Watanzania wamechoka kuumia na kuona nchi za
jirani hata zile ambazo hazikuwa na uwezo kama wan chi yetu zikifanya vizuri.
Nchi za jirani ziko kwenye mipango ya
kucheza Kombe la Mataifa Afrika, sasa ndiyo TFF ingekuwa inajiandaa na kuachana
na tabia ya kuamini mechi za kirafiki ndiyo saizi ya Watanzania na kwa kuwa
mechi hizo zitaingiza fedha kwa shirikisho hilo.
Kama inataka fedha zaidi iwe na mikakati
sasa ili kuandaa timu itakayocheza vema kwenye michuano ya awali ya Kombe la
Dunia na lile la Mataifa Afrika hapo baadaye.
Kwa sasa sisi ni Watanzania watazamaji, TFF
inahusika, iache kutuzuga au kupoteza muda eti kuna watu walihujumu timu,
badala yake ianze kupanga mikakati sasa.
Ingalie timu za taifa za vijana na si kwa
kulazimisha kuchukua fedha za wadhamini wa klabu. Iwe na ubunifu angalau kidogo
kama ile TFF ya Leodeger Tenga iliyopata udhamini kwenye timu kubwa ya taifa na
leo TFF ya Malinzi inautumia.
Isilale, isiwe laini, isiwe ngumu kufikiri,
nyepesi kulaumu. TFF ya Malinzi kwa kuwa ina kitengo cha masoko, basi isilipe
mishahara bure, watu wake wafanye kazi na kusaidia kupatikana kwa wadhamini.
Kupora fedha za wadhamini wa klabu,
kuzitumia eti kuendeleza timu za taifa ni mipango iliyopitwa na wakati kwa kuwa
utaua mizizi kwa madai unataka kumwagilizia mashinda. Kwani kuna wachezaji wa
timu ya taifa? Hao wanaokwenda timu ya taifa kwani wanatokea wapi, si kwenye
klabu, sasa kipi ambacho hamuelewi?
Kwani wewe Saleh unapamba nini kama si uzushi na uzandiki kwa kutumia kijarida chako cha jembe?
ReplyDeleteWewe huna tofauti na wale wanaoitwa simba Ukawa ambao kazi yao kuwabadilishia matokeo akina Aveva,nasikia nawewe upo miongoni mwao maana hata kadi yako inajionyesha!
Acha majungu kijana piga kazi wenzio akina Shaffih wanakula pesa wewe mikelele tuuu!