Waamuzi
kutoka Rwanda ndiyo watakaochezesha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Benin itakayofanyika Jumapili
(Oktoba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hakizimana
Louis ndiye atakayeongoza waamuzi hao wa FIFA kwa kupuliza filimbi kwenye mechi
hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.
Atasaidiwa na Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
Mechi
hiyo itatanguliwa na ile ya viongozi wa dini- Kiislamu vs Kikristo kudumumisha
upendo, amani na ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili alasiri. Tiketi za
elektroniki zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio
cha sh. 4,000 na sh. 10,000.
Wakati
huo huo, Kocha Mart Nooij ameongeza wachezaji watatu kwenye kikosi cha Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ili kukiongezea nguvu kwa
ajili ya mechi hiyo.
Wachezaji
walioongezwa ni Jonas Mkude na Joram Mgeveke kutoka timu ya Simba, na Gadiel
Michael wa Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment