RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI (KUSHOTO) AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU. |
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limefahamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) kuwa Tanzania haitaweza kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika- AFCON
2017 kwa kuwa haijawahi kuandaa fainali zozote za vijana Afrika. Fainali hizo
ni zile za vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20.
Hivyo, TFF inaelekeza nguvu zote katika kuandaa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka U17 mwaka 2019.
Tunapenda
kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Jakaya
Kikwete kwa kututia moyo katika kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
Pia
tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella
Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania kuomba
uenyeji wa AFCON 2017.
TFF inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment