November 30, 2014


Simba haitamtumia mshambuliaji wake, Paul Kiongera katika msimu huu.

Unaweza kusema imemtema kwani Simba imefikia uamuzi huo na Kiongera.

Kiongera anaweza kuondoka kesho kwenda India kwa matibabu ya goti.
Licha ya kwamba wiki iliyopita alitoa kali kwa kusema haijui safari ya India wakati amekuwa akienda mara kadhaa ubalozi wa India kufuata viza, sasa anaondoka kwenda kutibiwa.

Taarifa zinasema, Simba imelazimika kumuacha baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji Mganda, Danny Sserunkuma.

"Ni kweli hatutakuwa na Kiongera, anatakiwa kupumzika baada ya matibabu. Hivyo lazima tuitumie nafasi yake," kilieleza chanzo.

Mshambuliaji huyo raia wa Kenya aliumia katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic