November 30, 2014

NJOVU (KULIA) AKIWA NA ALIYEKUWA BOSI WAKE, MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MANJI.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu ambaye anamalizia muda wake, amesema anawashukuru wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.


Njovu amesema anawashukuru kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa Jangwani.

"Yanga ni klabu kubwa, changamoto ni nyingi sana. Lakini nawashukuru wanachama na mashabiki kwa ushirikiano wao.

"Nitaendelea kuwa mwanachama wa Yanga tena mwaminifu. Nimejifunza mengi, lakini sasa ni wakati wa kukabili changamoto nyingine," alisema Njovu.

Njovu amekuwa mmoja wa makatibu wa Yanga waliofanya vizuri katika kipindi wakiwa madarakani.

Ameamua kutoongeza mkataba baada ya ule aliokuwa nao kwisha muda wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic