Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema ile kauli aliyowahi kuitoa
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ndiyo imesababisha Yanga imkose kiungo Jonas
Mkude.
Hans Poppe amesema kauli
aliyowahi kuitoa Manji kuwa atawasajili wachezaji wa Yanga na kuwaacha wafanye
mazoezi kwenye michanga ya ufukwe wa Coco Beach ndiyo imesababisha Mkude aone
atapoteza kipaji chake.
“Huenda Yanga wangeweza
kumpata huyu kijana, lakini sasa kama Manji alisema wachezaji wa Simba anaweza
kuwasajili na kuwaacha wacheze mchangani ufukweni, Mkude akaona haitakuwa sawa.
“Hivyo ameamua kubaki
nyumbani na sisi sasa tunaelekeza nguvu kwa kijana wetu Msuva, tutaandika barua
ili Yanga watupe nafasi ya kuzungumza naye,” alisema Hans Poppe.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa
Yanga, Beno Njovu alipinga kauli hiyo ya Hans Poppe akisema hawakuwahi kuwa na
mpango wa kumsajili Mkude.
“Hatukuwahi kuwaza hivyo,
hayo ni mambo ya magazeti,” alisema Beno.
Hata hivyo, taarifa za
ndani kutoka Yanga zinaeleza, kweli Yanga ilikuwa inammezea mate kiungo huyo
lakini baada ya kuongezewa mkaaba wa miaka miwili na Simba, imeamua kuingia
kwenye kale ka wimbo ka “Sizitaki mbicho hizi.”
Salehe umezidisha mapenzi mpaka kwenye blog,unatuboa
ReplyDelete