KALI (KULIA) AIKUMBATIANA NA KOCHA MKUU WA YANGA, MARCIO MAXIMO. |
Kocha Msaidizi
wa Azam FC, Kali Ongala, amebwaga manyanga kuifundisha timu hiyo ambayo ni
bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Bara.
Kali,
ambaye alijiunga na Azam kama mchezaji na baadaye kupandishwa na kuwa kocha
msaidizi, juzi Jumatatu alitangaza kuachana na timu hiyo akisema kuwa anataka
kwenda kuongeza elimu yake ya ukocha nchini Uingereza.
Msimu
uliopita, Kali aliponea tundu la sindano kutimuliwa klabuni hapo, baada ya
aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall, kufungashiwa virago
vyake kutokana na uongozi kutoridhishwa na utendaji wake ambapo nafasi yake
ilichukuliwa na Mcameroon, Joseph Omog.
Kali amesema
kuwa ameamua kuachana na Azam kwa sababu anataka kwenda kuongeza elimu ya
ukocha nchini Uingereza na atachukua muda mrefu.
“Sijaondoka
kwa sababu timu imefungwa mechi mbili ila nimefikia hatua hiyo kwa sababu
nataka kwenda kuongeza elimu ya soka nchini Uingereza ambako nitatumia muda
mrefu,” alisema Kali.
Naye Katibu
Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassoro, aliliambia gazeti hii kuwa, tayari
wameshapata mrithi wa nafasi hiyo iliyoachwa na Kali.
“Kuanzia
sasa Ibrahim Shikanda ndiye atakayekuwa kocha wetu msaidizi mpaka hapo Kali
atakapomaliza masomo yake japokuwa hatujui atamaliza lini,” alisema Nassor.
Shikanda
ambaye ni raia wa Kenya, aliwahi kuitumikia klabu hiyo akiwa kama mchezaji na
nahodha.
0 COMMENTS:
Post a Comment