November 5, 2014

MAXIME
Wakati uongozi wa Simba uko katika utatuzi wa sakata la wachezaji wake watatu Haruna Chanongo, Amri Kiemba na Shabani Kisiga, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amesema kuwa anawahitaji nyota hao.

Hivi karibuni uongozi wa Simba uliwasimamisha wachezaji hao kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, wakidaiwa kuufanya wakati walipokuwa mkoani Mbeya na kikosi cha timu hiyo lakini juzi waliitwa na kuhojiwa na hukumu yao inatarajiwa kutoka leo.

Maxime amesema kuwa kama Simba haina tena mpango wa kuendelea na wachezaji hao katika kikosi chake, basi yeye yupo tayari kuwachukua.
“Wachezaji hao ni wazuri na hakuna mtu yeyote anayeweza kupinga juu ya hilo, hivyo kama Simba watawaacha nipo tayari kuwachukua.
“Kama wana matatizo ya nidhamu, hilo ni jambo la kawaida ambalo linarekebishika, hivyo wakija kwangu nina imani watarekebishika na watafanya kazi yao kwa amani zaidi,” alisema Maxime.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic