November 22, 2014


SIKU JAJA ALIPOWASILI NCHINI

Jaja hatarejea nchini kukipiga Yanga na badala yake Kocha Marcio Maximo ameamua kutafuta mbadala.


Kiungo mkabaji raia wa Brazil Emerson De Oliveira Neves Rouqe anatarajiwa kuwasili siku ya Jumanne mchana jijini Dar es salaam kufanya majaribio Jangwani.

Emerson aliyezaliwa miaka 24 iliyopita jijini Rio de Janeiro, Brazil atawasili nchini akiongozana na Kocha Marcio Maximo ambaye alikuwa mapumziko nchini humo.
Iwapo atafanikiwa katika majaribio hayo, katika klabu ya Young Africans, basi atajumuishwa katika listi ya wachezaji watakaokipiga Yanga msimu huu.

 na endapo atafuzu moja kwa moja atajiunga na mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic