Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa Ligi Daraja la Pili (SDL)
huku ikikata majina mawili ya wachezaji katika klabu za Abajalo ya Dar es
Salaam na Magereza ya Iringa.
Klabu
hizo mbili zilisajili wachezaji 31 badala ya 30 ambapo ni kinyume na Kanuni ya
61(2) ya Ligi Daraja la Pili inayoruhusu klabu kusajili wachezaji wasiozidi 30
na wasiopungua 18.
Wachezaji
ambao Kamati ya Sheria iliyokutana jana (Novemba 11 mwaka huu) imewaondoa ni
wale waliokuwa wameorodheshwa namba 31 katika usajili wa klabu hizo. Wachezaji
hao ni Andrew Mathew Kazembe (Abajalo) na Joshua Omari (Magereza).
Michuano
ya Ligi Daraja la Pili inayoshirikisha timu 24 katika makundi manne ya timu
sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka
huu.
Wachezaji
waliopitishwa katika kila klabu na idadi yao kwenye mabano ni Abajalo (30),
Arusha FC (18), Bulyanhulu (28), Kariakoo (30), Kiluvya United (23), Magereza
(30), Mbao (27), Milambo (29), Mji Mkuu (29) na Mkamba Rangers (30).
Wengine
ni Mpanda United (29), Mshikamano (28), Mvuvumwa (18), Njombe Mji (25), Pamba
(24), Rwamkoma JKT (25), Singida United (26), Town Small Boys (22), Transit
Camp (28), Ujenzi Rukwa (30), Volcano (25) na Wenda (20).
Klabu
zote zinakumbushwa kulipia na kuchukua leseni za wachezaji wao kabla ya ligi
kuanza, kwani kwa mujibu wa kanuni hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kucheza
mechi ya ligi bila kuonyesha leseni yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment