MKWASA |
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imeunda jopo la watu watano kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki hatua ya
ngazi ya Taifa ya michuano ya Copa Coca-Cola 2014.
Michuano
hiyo ya ngazi ya Taifa itafanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 13 hadi 20
mwaka huu. Uhakiki wa umri utafanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu wakati timu
zote zinatakiwa kuwasili Shule ya Filbert Bayi mkoani Pwani kuanzia Desemba 10
mwaka huu.
Jopo
hilo la uhakiki linaongozwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Henry Tandau. Wengine katika jopo hilo ni Ally Mayay, Charles
Boniface Mkwasa, Dk. Jonas Tiboroha na Richard Yomba.
Timu
16 zitakazocheza michuano hiyo inayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka
15 ni Arusha, Dodoma, Geita, Katavi, Kigoma, Kinondoni, Kusini Pemba, Kusini
Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Simiyu na
Tanga.
Vyama
vya mpira wa miguu vya mikoa vinakumbushwa kutuma TFF fomu za usajili ambazo
zinatakiwa kuambatanishwa vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji husika.
0 COMMENTS:
Post a Comment