November 25, 2014


Wakati Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri akiwa mapumzikoni kwao Zambia, msaidizi wake, Selemani Matola ameanza kupiga kazi.


Matola ameanza kuwanoa wachezaji wake gym pamoja na uwanjani.
Leo asubuhi, Simba walifanya mazoezi kwa saa tatu katika gym.

Baada ya mazoezi makali wakati wakiamini wamemaliza, Matola aliwachukua na kuwapeleka uwanjani.
Wakiwa kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe, Simba walijifua kwa saa zima.
Maana yake kwa siku tayari walikuwa wamejifua kwa saa nne.



Simba inaaza kujiweka sawa baada ya likizo fupi, ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na ile mechi ya bonanza la mwezi ujao dhidi ya watani wao Yanga.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic