November 25, 2014


NAFASI ZA SCHOLARSHIP 2015.
DAORA SCHOOL inapenda kuwatangazia kuwa itaendelea na mpango wako wa kutoa scholarship kwa wanafunzi kama sehemu ya juhudi za kusaidia jamii kupitia sekta ya elimu. Katika mwaka 2014 DAORA SCHOOL ilitoa scholarship kwa wanafunzi 17 ambao walikuwa na uhitaji na walifaulu mtihani wa utimamu ulioandaliwa na shule.


Katika mwaka 2015 DAORA SCHOOL itatoa scholarship kwa wanafunzi 6 wa kidato cha pili na kwanza kwa masharti yafuatayo:
1.   Mwombaji lazima awe ametembelea ukurasa wa facebook was DAORA SCHOOL na kulike ukurasa huo. Unaweza kupitia ukurasa wa facebook kwa baada ya kutembelea tovuti ya shule: www.daoraschool.ac.tz
2.   Tuma maombi yako ya kufanya mtihani wa utimamu utakaondaliwa na shule kupitia barua pepe: daoraschool@yahoo.com au info@daoraschool.ac.tz au sms kupitia namba: 0737213524, 0737213525, 0737213526.

3.   Mwombaji lazima ajaze fomu ya usajili wa wanafunzi inayopatikana katika tovuti ya shule; www.daoraschool.ac.tz na kuzituma kwa barua pepe hapo juu au kwa njia ya posta au kuleta shueni moja kwa moja.

4.   Mtihani wa utimamu utafanyika tarehe 10 Januari 2015.
5.   Mwombaji lazima alipe ada ya mtihani ya Tshs. 20,000/- ambayo inajumuisha gharama za mtihani, chai na chakula cha mchana. Gharama hizo zinaweza kulipwa benki, Daora School, A/C No. 0150237207100, CRDB Bank, Holland House Branch au malipo taslimu shuleni kwa mhasibu. Endapo malipo yatafanyika benki, lazima mwombaji aje na stakabadhi ya benki.

Matokeo yatatangazwa siku hiyo hiyo.
Kwa maelezo zaidi tembelea: www.daoraschool.ac.tz au piga simu 0737213524, 0737213525, 0737213526.

Imetolewa na DAORA School.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic