Mshambuliaji wa zamani wa
Simba, Betram Mwombeki, amesajiliwa rasmi katika kikosi cha maafande wa Ruvu
Shooting kwa muda wa mwaka mmoja.
Straika huyo msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba
akitokea Pamba na aliweza kufanya vyema katika mzunguko wa kwanza lakini wa
pili hakuweza kupata nafasi ya uhakika, hivyo akaumaliza msimu akiwa na mabao
manne tu.
Msemaji wa Ruvu Shooting,
MAsau Bwire amethibitisha hilo lakini akataka apewe siku moja ili kulizungumzia
hilo hadharani.
“Ni kweli tuko katika
harakati za kuimarisha safu ya ushambuliaji na Mwombeki tutampa mwaka mmoja,”
alisema Bwire.
Baada ya kuondoka Simba, Mwombeki
alikwenda Oman na kufanya majaribio katika kikosi cha Oman Club FC
linachoshiriki daraja la kwanza. Lakini akafeli.
Nenda kasafishe Nyota, Simba haohao kesho watakuja na Minoti. Ndo soka la kibongo No subira No uvumilivu! Kwanza Ruvu hautakuwa na stress za mashabiki!
ReplyDelete