KIONGERA |
Mshambuliaji Paul ‘Modo’ Kiongera wa Simba,
sasa ameingia kwenye mstari mwekundu wa wale ambao wanaweza kuachwa kwenye
kikosi hicho.
Simba inafanya kila linalowezekana kupitia
dirisha dogo, ili iimarishe kikosi chake.
Kiongera raia wa Kenya aliyeonekana ana uwezo
mkubwa wa kufunga mabao, ameingia kwenye kundi la wanaoweza kutemwa kutokana na
kuwa majeruhi.
“Kama atakuwa majeruhi kwa muda mrefu,
hakutakuwa na ujanja, ataachwa,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.
Simba inahitaji nafasi za kuwaongeza Emeh Izuchukwu
anayekipiga nchini Norway na Danny Sserunkuma kutoka Gor Mahia ya Kenya.
Inaonekana kama Kiongera hatakuwa na msaada na
Simba na taarifa zinasema, ripoti ya daktari ndiyo itakayoamua.
Uchunguzi wa Championi Jumatano unaonyesha
iwapo atatakiwa kupumzika hadi miezi mitano, basi nafasi yake itakwenda kwa
Sserunkuma.
Baada ya hapo, bado Simba itaendelea kusaka
nafasi ya pili iwapo itakubaliana na Izuchukwu. Hapa ni zamu ya Pierre Kwizera
au Amissi Tambwe.
Kitaalamu kunaonekana kuna mkanganyiko, mkataba
wa nahodha Joseph Owino unakwisha. Simba wanaendelea kujiuliza kuhusiana na
kiwango chake.
Mjadala ni kumuacha Kwizera kwa kuwa akiumia
Jonas Mkude itakuwaje? Pia ikiwa kocha mpya atataka ‘holding midfield’ wawili
kama ilivyokuwa kwa Zdravko Logarusic, itakuwa vipi? Inachanganya.
Bado swali linakuja kuwa basi aachwe Tambwe!
Simba bado wanajiuliza yeye ndiye mfungaji bora msimu uliopita. Utaona bado
inachanganya kwao lakini muda utaeleza.
Tatizo la kuunda timu za msimu litaendelea kutugharimu ma kupoteza mamilioni ya fedha za timu/wafadhili! Kiongera kaumia katika timu na bado anaonekana ana kipaji cha kufunga lakini majeruhi yanamfanya awe mbuzi wa kafara! WHY! Hao watakaoletwa nao wakiboronga na Mungu jaalia Kiongera kapona mnaenda kumpigia magoti kama ilivyokuwa kwa Owino J. Ni umburura, Kiongera atibiwe afanye kazi haina haja kumvunjia mkataba!
ReplyDelete