November 30, 2014


Benchi la ufundi la Simba, limeandaa mechi maalum ya timu yake ya wakubwa dhidi ya ile ya B.
Uamuzi wa kuandaa mechi hiyo ni kutaka kupata wale watakaopandishwa kwenye kikosi cha kwanza.

Lakini pia kutaka kufanya muendelezo mpya wa kikosi cha timu ya vijana.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo na kusisitiza itakuwa ni muhimu kwa kikosi chake.

“Kweli itakuwepo na tutacheza kule mazoezini Boko. Wachezaji wanajua kuhusiana na mechi hiyo, ni muhimu sana,” alisema Phiri.

Simba ni kati ya timu zenye vikosi bora vya timu B ambayo awali ilikuwa inanolewa na Selemani Matola.

Kwa sasa Matola ni kocha msaidizi na kikosi hicho kinanolewa na Nico Kiondo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic