November 29, 2014

TAMBWE AKISHUKA KWENYE GARI YAKE AINA YA TOYOTA MARK X BAADA YA KUWASILI MAZOEZINI.

Straika wa Simba aliyevuma msimu uliopita, Amissi Tambwe, amekuja kivingine wakati huu akitoka likizo fupi baada ya kushusha ‘ndinga’ mpya kutoka kwao Burundi.

Gari hili aina ya Toyota Mark X litakuwa likilipiwa dola  300 (Sh 521,539) kwa mwaka kwa kuwa linatumia  ‘number plate’ ya Burundi.


Gharama hizo zinatokana na nyota huyo kutokuwa tayari kubadili namba ya usajili wa gari lake aina ya Toyota Mark X 250G yenye namba za Burundi I A 2336, ambapo anatumia ya nchini kwao Burundi, ambapo analazimika kuilipia kiasi cha dola 25 (Sh 43,461) kila mwezi, sawa na dola 300 kwa mwaka.


Akizungumza na SALEHJEMBE, Tambwe amesema:

“Ni kweli ni mpya, nilitoka nayo nyumbani (Burundi) nilipokwenda likizo fupi. Ujue niliiagiza mapema kabla hatujakwenda mapumziko, kwa hiyo niliamua kuja nayo huku, maana ndiyo lilikuwa lengo langu kuileta Bongo,” alisema Tambwe.


Gari hilo linakadiriwa kuwa na thamani ya kati ya Sh milioni 32 hadi 35 kwa hapa Bongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic