November 29, 2014

HIMID (KUSHOTO) AKIITUMIKIA AZAM FC..
Beki wa Mwadui FC, Juma Jabu wa Mwadui na kiungo wa Azam FC, Himid Mao wa Azam wameshindwa kuikoa timu yao ya 'kitaa'.

Licha ya uwepo wao katika kikosi cha Kagera Rangers, walijikuta wakishindwa kukisaidia kuibuka na ushindi dhidi ya Saigon baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ya mchangani, Kagera Rangers ilimenyana na Saigon katika mchezo wa mashindano ya Tarimba Rangers Cup.

Mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Shule ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.


Mabao ya Saigon yalifungwa na  Mohammed Mkopi, Ally Karuu na Issa Kanduru huku la kufutia machozi la Saigon likifungwa na Juma Jabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic